TEZI DUME NI NINI - KIDEKAFITNESS

Breaking

Post Top Ad

Friday 19 November 2021

TEZI DUME NI NINI

 TEZI DUME NI NINI

Hii ni tezi (kokwa) ambayo inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa ni kutengeneza maji maji ya uzazi kwa mwanaume (shahawa) ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizotengenezwa kutoka kwenye korodani na husaidia kusafirisha mbegu za kiume na kuzifanya zibaki hai kwa muda unaostahili.




Tezi hii huwa inaongezeka uzito au ukubwa kadri umri wako unavyozidi kukua. Na nimekwambia kuwa tezi hii ipo katika shingo ya kibofu cha mkojo na hivyo basi ukuaji wake unaweza kuathiri mfumo mzima wa utoaji mkojo kwenye kibofu(Incomplete bladder emptying) .


Tafiti zinaonesha kwamba tezi huanza kuongezeka uzito kuanzia miaka 25, na huendelea kukua kila siku kadri umri unavyo enda. Kuongezeka kwa uzito wa tezi yako ya kiume sio tatizo kimatibabu kwani kipimo cha kuonesha moja kwa moja umefikia hatua sio nzuri ni pale unapoanza kupata dalili zenye kuzuia mkojo kutotoka vizuri (obstructive symptoms).


Hivyo uzuri ni kwamba kuanzia pale tezi inapokuwa inaongezeka ukubwa hadi kufikia kuonesha dalili mbaya ni hadi unapofikia angalau umri wa miaka 60 na kuendelea , pia inaweza hata ikatokea hata unapokuwa una umri chini ya miaka 50 inategemea na mwili wako kibaolojia. 


Basi kukua huku kwa tezi bila sababu ya msingi tunaweza tukawa na hitimisho la magonjwa makuu mawili au matatu,Kwanza Benign Prostate Hypertrophy (BPH) aka Kukua kwa tezi dume, pili Prostate cancer Hii ni kansa ya tezi dume na Tatu Uvimbe kwenye kibofu cha mkojo.


Njia pekee ya kuyatenganisha magonjwa hayo matatu kwa wanaume ni kwa njia kuu mbili, Kwanza Chukua historia vizuri ya mgonjwa wako kuanzia alipo anza kuona dalili na angalia afya yake vzuri kabisa,Afya ni muhimu sana kwani moja ya dalili ya moja kwa moja ya kubaini kuwa mtu ana kansa ni kudhoofika kwa mwili wake, Hivyo historia ya mgonjwa ni muhimu sana.


Mfano, Mgonjwa wa kuvimba kwa tezi dume atakuja ana umri wa miaka 69 analalamika mkojo unatoka kwa kudondoka kama matone matone hautoki katika mfululizo, pia anakwambia mkojo unakuwa unabaki kwenye kibofu na analalamika kiuno kinamuuma sana na UTI za mara kwa mara lakini ukimwangalia afya yake ipo vizuri hajadhoofika kwa lolote. Hivyo basi mgonjwa huyu moja kwa moja anakuwa ameangukia kwenye BPH na sio kansa ya tezi dume.


Mfano mwingine Anakuja mzee wa miaka 85 amedhoofika afya yake mbavu zote na mifupa ya usoni ipo nje, analalamika kuwa mkojo hautoki vizuri, anakojoa mara kwa mara na hamalizi mkojo wote kwenye kibofu na UTI za mara kwa mara, Hapo lazima akili yako impeleke mgonjwa wako kuwa ana Prostate Cancer.


Wagonjwa wengi pia wanaweza wakaja na dalili za uvimbe kwenye kibofu (bladder tumor) huwezi kubaini uvimbe kwenye kibofu kwa kupiga kipimo cha picha yoyote bali njia pekee ni kuchukua sampuli ya kipande cha uvimbe kwa kusaidiwa na kipimo kiitwacho Cystoscope (kipimo kinachopiga picha kibofu cha mkojo na kuona uvimbe live kwa kutumia screen iliyopo pembeni mwa mtaalamu wa vipimo.


Moja ya dalili ambazo mgonjwa wa namna hii anaweza kukueleza ni kukojoa mara kwa mara ( Uvimbe kwenye kibofu unapunguza ukubwa wa kibofu hivyo kibofu kinajaa mara kwa mara) Pia wengi huja wakilalamika kuwa wanakuwa na historia ya kukojoa damu mwishoni anapokuwa anamalizia kusukuma 




Watu wengi wamekuwa wakiniuliza swali kama hili

Eti hivi tezi dume ni sawa na mshipa wa ngiri (hernia)?


Napenda kukujibu kuwa hivyo ni vitu tofauti kabisa na matibabu yake tofauti kabisa. Kutokana na elimu ya tiba ya kizungu (convetional medicine) ugonjwa wa mshipa wa ngiri ni ugonjwa unahitaji operation kulingana na ngazi ugonjwa huo umefikia wapi ( Nitaeleza kidogo).


Hernia kwa lugha nyepesi ni ile hali ya viungo vya tumboni kujitokeza nje pamoja pamoja na ngozi na kutengeneza kama mfuko flani unaoning’inia. Kutokeza huku kuneweza kukawa kupitia kitovu , pembeni ya kitovu au sehemu za siri (Inguinal hernia au ngiri). inategemeana imetokea wapi


Hivyo kuna viungo ambavyo unaweza kujaribu kuvirudisha ndani vikakubali na baada ya muda, labda umekohoa vinatokeza tena (Reducible Hernia) na kuna hernia ambayo huwezi kuirudisha ikisha tokeza imetokeza ( Non reducible hernia).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages